Imani za Msingi wa Waadventista Wa Sabato

1. Maandiko Matakatifu

Maandiko Matakatifu, yaani Agano la kale na Jipya ndiyo Neno la Mungu lililoandikwa,likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia kwa watu watakatifu walionena na kuandika kama walivyoagizwa na Roho Mtakatifu. Ndani ya neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu maarifa yaliyo lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa wa mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye mamlaka wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya mungu katika historia.(2Petro 1:20,21. 2Timotheo 3:16,17. Zaburi 119: 105. Mithali 30: 5,6. Isaya 8:20. Yoh 17:17. 1 Wathesalonike 2:13. Waeb 4:12.)

2. Utatu Matakatifu

Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, umoja wa nafsi tatu za milele. Mungu hapatikani na mauti, mwenye nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko daima. Yeye hana mwisho na ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika kupitia kujifunua kwake binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, kutumikiwa na viumbe vyote. (Kumb 6:4. Mithali 28:19. 2 Kor 13:14. Waef 4:4-6. 1 Petro 1:2 1 Tim 1:17 Ufunuo 14:7)

3. Baba

Mungu Baba wa milele ndiye muumbaji, Chimbuko, Mtengenezaji, na Mfalme wa viumbe wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, Mwingi wa rehema,, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, na mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu. Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni ufunuo wa Baba. (Mwanzo 1:1 Ufu 4:11. 1 Wakor 15:28. Yoh 3:16. 1 Yoh 4:8. 1 Tim 1:17. Kut 34:6,7. Yoh 14:9)

4. Mwana

Mungu Mwana wa milele alifanya mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote viliumbwa, tabia ya mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakaribishwa na ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli, Yesu aliye kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa na bikira Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu majaribu kama mwanadamu, lakini kwa ukamilifu alioonyesha kwa mfano wa haki na upendo wa Mungu. Kwa miujiza yake alidhihirisha uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa. Aliteseka na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kama mbadala wetu, Alifufuliwa kutoka kwa wafu, na akapaa kuhudumu katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika utukufu kwa ajili ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh 1: 1-3,14. Wakol 1: 15-19,. Wafil 2:5-11. Yoh 10:30, 14:9 Warum 6:23. 2 Wakor 5:17-19.Yoh 5:22. 1 Wakor 15:3,4. Luka 1:35. Yoh 14:1-3)

5. Roho Mtakatifu

Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji, kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu. Alijaza maisha ya kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa, huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko uliongoza kwenye ukweli wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2 Petr 1:21. 2 Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26, 15:26,27, 16:7-13)

6. Uumbaji

Mungu ni muumba wa vitu vyote, na amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio la shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “Mbingu na Nchi” na vitu vyote vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji. Mwanaume na Mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa kazi yake ya Uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuajibika na utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana” ukitangaza utukufu wa Mungu. (Mwa 1,2. Kut20:8-11. Zab 19:1-6, 33:6-9, 104. Waebr 11:3)

7. Asili Ya Mwanadamu

Mwanaume na Mwanamke walifanyawa kwa mfano wa Mungu wakiwa kila mmoja na nafsi yake, uwezo na uhuru wa kufikirina kutenda. Ingawa waliumbwa viumbe huru, kila mmoja ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili, akili na roho, akimtegemea Mungu kwa uhai na pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka kutoka hadhi yao ya juuchini ya Mungu. Sura ya Mungu iliyopo ndani yao ikaharibika na wakawa chini ya mauti. Wazao wao hushiriki asili hii ya kuanguka na matokeo yake. Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya kuelekea kwenye uovu. Lakini Mungu katika kristo aliupatanisha ulimwengu na nafsi yake, na kwa Roho wake hurejesha ndani ya mwanadamu watubuo sura ya muumba wao. Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukufu wa Mungu, wanaitwa kumpenda na kupendana wao kwa wao na kutunza mazingira yao.(Mwa 1:26-28, 2:7. Zab 8:4-8. Mdo 17:24-28. Mwa 3. Zab 51:5 War 5:12:17. 1 Yoh 4:7,8,11,20. Mwa 2:15

8. Pambano Kuu

Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina ya kristo na shetani kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya ulimwengu. Ugomvi huu ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa uhuru wa kuchagua, katika kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na kupelekea sehemu ya Malaika kwenye uasi. Akaiagiza Roho ya uasi katika ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa kingia dhambini. Dhambi hii ya mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji ya sura ya Mungukatika wanadamu, Uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea wakati wa gharika iliyokumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote ulimwengu huu ukawa uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo hatimaye akathibitika kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano hili, kristo anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na kutegemeza katika njia ya wokovu. (Ufu 12:4-9, Isa 14:12-14, Eze 28:12-18, War 1:19-32, 5:12-21, 8:19-22, 1 Wakor 4:9, Waeb 1:14)

9. Maisha, Mauti na Ufufuo wa kristo

Mungu ni muumba wa vitu vyote, na amefunua katika maandiko uhalisi wa tukio la shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya “Mbingu na Nchi” na vitu vyote vilivyoko hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba ya juma lile la kwanza. Na hivyo akaanzisha sabato kama kumbukumbu ya milele ya kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji. Mwanaume na Mwanamke wa kwanza walifanywa kwa mfano wa Mungu kama upeo wa kazi yake ya Uumbaji, wakapewa utawala juu ya ulimwengu, na wakaagizwa kuajibika na utunzaji wake. Wakati ulimwengu ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana” ukitangaza utukufu wa Mungu. (Mwa 1,2. Kut 20:8-11. Zab 19:1-6, 33:6-9, 104. Waebr 11:3)

10. Uzoefu wa Wokovu

Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya Kristo, asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwamba katika yeye tuweze kufanywa haki ya Mungu. Tukiongozwa na Roho mtakatifu tunatambua hitaji letu, tunakili hali yetu ya kuwa wenye dhambi, tunatubu maasi yetu, na kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana na Kristo, kama mbadala na kielelezo. Imani hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa kimbingu wana ni karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa kristo tunahesabiwa haki, tunafanywa kuwa wana wa binti za Mungu, na kukomesabiwa haki kutoka katika hali ya kuwa chini ya dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upya na kutakaswa, Roho hufanywa upya nia zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washiriki wa asili ya uungu na tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu. (2 Wakor 5:17-21, Yoh 3:16, Wag 1: 4, 4:4- 7, Tito 3:3-7, Yoh 16:8, Wag 3:13,14. 1 Petr 2:21,22. Warumi 10:17, 3:21-26, 8:14-17, 12:2. Warumi 8:1-4,5:6-10, 2 Petro 1:3,4)

11. Kukua Katika Kristo

Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye aliyewatiisha pepo wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu zao na kuthibitisha mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu utupatia ushindi dhidi ya nguvu za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala, tunapo tembea naye kwa amani, furaha, na uhakika wa upendo wake.Sasa Roho Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu. Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yetu tunawekwa huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya nguvu za uovu, ujinga, na katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali,. Katika uhuru huu mpya ndani ya kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea naye kila siku katika sala, na kujilisha neno lake kikamilifu, tukikusanyika pamoja kwa ajili ya ibada, na kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo wale wanaotuzunguka na kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa njia ya Roho hugeuza kila wasaa na kazi kuwa uzoefu wa kiroho. (Zab 1:1,2. 23:4, 77:11,12, Kol 1:13-14, 2:6, 14-15, Luka 10:17-20, Efe 5:19-20, 6:12-18, 1 Theo 5:23, 2 Petr 2:9, 3:18. Fil 3:7-14, Math 20:25-28, Yoh 20:21, Gal 5:22-25, Rum 8: 38-39, 1 Yoh 4:4, Ebr 10)

12. Kanisa

Kanisa ni jamii ya waumini wanaomkiri Yesu kristo kuwa Bwana na mwokozi katika mfululizo wa kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za agano la kale, tunaitwa kutoka katika ulimwengu, na tunajiunga pamoja kwa ajili ya ibada, kwa ajili ya ushirika, kwa ajili ya mafundisho katika neno, na kwa ajili ya maadhimisho ya meza ya bwana, kwa ajili ya huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni kote, kanisa linapata mamlaka yake kutoka kwa kristo, aliye neno lililofanyika mwili, na kutoka katika maandiko, ambayo ndiyo neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya Mungu, waliofanywa nayeye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika misingi ya agano jipya. Kanisa ni mwili wa Kristo, jamii ya wenye imani ambayo kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi ambaye kwa ajili yake kristo apate kulisafisha na kulitakasa.Wakati wa kurudi kwake kwa ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewew kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne zote, walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu na lisilo na ila.(Mwa 12:3, Mdo:7:38, Waef 4:11-15, 3:8-11, Math 28:19,20, 16:13-20, 18:18, Waef 19:22,23, 5:23-27, Wakol 1:17-18).

13. Masalio na Utume Wake

Kanisa la ulimwengu lijumuisha wale wote ambao kwa kweli wanamwamini kristo, lakini katika siku za mwisho, kipindi cha kuenea kwa ukengeufu, masalio wameitwa kuzishika amri za Mungu na imani ya Yesu kristo. Masalio hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya hukumu, hutangaza wokovu kupitia kristo, na hupiga mbiu ya kukaribia kwa marejeo yake. Tangazo hili huwakilishwa katika mfano wa malaika watatu wa ufunuo 14, huambatana na kazi ya hukumu mbinguni na kuwa na matokeo ya kazi ya toba na matengenezo duniani. Kila muumini anatakiwa kuwa na sehemu binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni kote. (Ufu 12:17, 14:6-12, 18:1-4, 2 Wakor 5:10, Yuda 3,14, 1 Petro1:16-19, 3:10-14, Ufu 21:1-14)

14. Umoja Katika Mwili wa Kristo

Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki wengi, walioitwa kutoka katika taifa, kabila, lugha, na watu. Katika kristo tu viumbe wapya, ubainishi wa rangi, tamaduni, elimu, na taifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu naya chini, tajiri na maskini, mwanaume na mwanamke,havipaswi kuleta mgawanyiko miongoni mwetu.Sote tu sawa katika kristo, ambaye kwa roho mmoja ametufunga katika ushirika mmoja pamoja nayeye na sisi wenyewe kwa wenyewe, tunapaswa kutumika na kutumikiwa pasipo kupendelea au kusita. Kupitia kwa Yesu kristo katika maandiko tunashiriki imani na tumaini moja, na tunawafikia wote kwa ushuhuda mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu mmoja mwenye nafsi tatu, ambaye ametufanya sisi tu watoto wake.(War 12:4,5, 1 Wakor 12:12-14, Math 28:19,20, Zabr 133:1, 2 Wakor 5:16,17, Mdo 17:26,27, Waef 4:14-16, 4:1-6, Yoh 17:20-23)

15. Ubatizo

Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa Yesu kristo, na kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika upya wa maisha. Hivyo tunamkubali kristo kuwa Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu wake, na tunapokelewa kama washiriki wa kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa muungano wetu na kristo, msamaha wa dhambi zetu na kupokea kwetu Roho Mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa majini na unategemea uthibitisho wa imani katika yesu na ushindi wa toba ya dhambi. Unafuata mafunzo katika maandiko matakatifu na ukubali wa mafundisho yake. (Warum 6:1-6, Wakol 2:12,13, Mdo 16:30-33, 22:16, 2:38, Math 28:19-20)

16. Meza Ya Bwana

Meza ya Bwana ni ushiriki katika mfano wa mwili na damu ya Yesu kama udhihirisho wa imani katika yeye, Bwana na mwokozi wetu. Katika ushirika huu kristo anakuwepo kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadri tunavyoshiriki, kwa furaha tunatangaza mauti ya Bwana mpaka arudipo tena. Maandalizi kwa ajili ya meza ya Bwana hujumuisha kujihoji nafsi, toba na ungamo. Bwana aliamua huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha kutakaswa upya, kuonyesha nia ya kutumiana wenyewe kwa wenyewe katika unyenyekevu ufananao na wa kristo, na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya Meza ya Bwana wazi kwa waumini wote wakristo. (1 Wakor 10:16,17, 11:23-30, Math 26:17-30, Ufu 3:20, Yoh 6:48-63, 13:1-17)

17. Karama Za Roho na Huduma

Mungu huwakirimia washiriki wote wa kanisa lake katika kila kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo kwa ajili ya mema ya kawaida ya kanisa na wanadamu. Zikitolewa kwa wakala wa Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa na kanisa katika kuytekeleza shughuli zake zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na maandiko huduma hizi hujumuisha huduma kama: Imani, uponyaji, unabii, mahubiri, mafundisho, utawala, upatanisho, huruma, na huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya msaada na faraja kwa watu. Baadhi ya washiriki huitwa na mungu na kukirimiwa na Roho kwa ajili ya shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, na utume, na huduma za kufundisha zinahitajika hasa katika kuwapatia zana washiriki kwa ajili ya huduma kulijenga kanisa hadi ukomavu wa kiroho, na kukuza umoja wa imani na maarifa ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya mivuto miharibifu ya mafundisho ya uwongo, na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa Mungu, nakujengeka imara katika imani na upendo.(Warumi 12:4-8, 1 Wakor 12:9-11, 27,28. Waef 4:8,11, Mdo 6:1-7, 1 Petr 4:10-11)

18. Karama Ya Unabii

Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii, karama hii ni alama-kitambulisho cha kanisa la masalio na ilidhihirishwa katika huduma ya Ellen G. White. Kama mjumbe wa Bwana, maandishi yake ni chanzo kiendelezi na yenye mamlaka ya ukweli yanayolipatia kanisa faraja, uongozi, mafundisho, na maonyo. Pia yanaweka wazi kuwa Biblia ndiyo kanuni ambayo kwa hayo mafundisho yote na uzoefu lazima vipimwe. (Yoeli 2:28,29, Mdo2:14-21, Waeb 1:1-3, Ufu 12:17, 19:10)

19. Sheria Ya Mungu

Kanuni kuu za sheria ya Mungu zimetiwa pamoja katika Amri kumi na mfano wake ulidhihirishwa katika maisha ya kristo. Nazo zinadhihirisha upendo wa Mungu, mapenzi yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni sharti kwa watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo msingi wa agano la Mungu na watu wake na kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia uwakala wa Roho Mtakatifu zinasonda dhambi na kuhamsha hisia za hitaji la mwokozi. Wokovu wote ni katika neema, na si kwa matendo, lakini tunda lake ni utii wa amri kumi. Hutii huu hukuza tabia ya kikristo na huwa na matokeo ya ustawi. Ni ushuhuda wa upendo wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya wanadamu wenzetu. Utii wa imani udhihirisha uwezo wa kristo kubadilisha maisha, na hivyo huimarisha ushuhuda wa kristo. (Kut 20:1-17, Zab 40:7,8 Math 22:36-40 Kumb 28:1- 14 Math 5:17-20, War 8:3,4 Zab 19:7-14)

20. Sabato

Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za uumbaji, alipumzika siku ya saba na kuanzisha sabato kwa ajili ya watu wote kama kumbukumbu ya uumbaji. Amri ya nne ya sheria za Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la sabato hii ya siku ya saba kama siku ya mapumziko, ibada, na huduma kulingana na mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano yenye furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi. Ni mfano wa ukombozi wetu katika kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu, na mwonjo wa umilele wetu wa siku zijazo katika ufalme wa Mungu. Sabato na ishara ya daima ya mungu ya agano la milele la Mungu kati yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa wakati huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimishola matendoya Mungu ya uumbaji na ukombozi. (Mwa 2:1-3, Kut 20:8-11, Luka 4:16, Isay 56:5- 6, 58:13-14, Math 12:1-12, Ezek 20:12-20, Kumb 5:12-15, Wal 23:32, Marko 1:32).

21. Uwakili

Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa nayeye wakati na fursa, uwezo na mali, na mibaraka ya dunia na raslikamali zake. Tunawajibika kwake kwa matumizi yake sahihi. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya uaminifu kwake na kwa wanadamu wenzetu, na kwa kurudisha Dhaka na kutoa sadaka kwa ajili ya utangazaji wa injili yake na kwa utegemezaji na ukuaji wa kanisa lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika upendo na ushindi dhidi yao choyo na tama. Wakili kufurahia mibaraka inayowajia wengine kama matokeo ya uaminifu wake.(Mwa 1:26-28, 2:15, 1 Nyak 29:14, Hagai 1:3-11, Malaki 3:8-12, 1 Wakor 9:9-14, Math 23:23, 2 Wakor 8:1-15 Warumi 15:26-27.)

22. Mwenendo Wa Kikristo

Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri, kujisikia, na kutenda kutenda kulingana na kanuni za mbinguni. Ili Roho aumba ndani upya ndini yetu tabia ya Bwana wetu tunajihusisha tu katika mambo yale ambayo yatazaa katika maisha yetu usafi unaofanana na kristo, afya, na furaha katika maisha yetu. Hii inamaanisha kwamba maraha na maburudisho yetu yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji na uzuri wa kikristo. Huku tukitambua tofauti za kitamaduni, mavazi yetu yanapaswa yawe ya kawaida, si ya anasa, na safi, yanayostahili wale ambao uzuri wao wa asili yake si mapambo ya nje, bali asili yake ni mapambo yasiyoharibika, yenye roho ya upole na utulivu. Pia inamaanisha kwamba kwa kuwa miili yetu ni mahekalu ya Roho mtakatifu, tunapaswa kuitunza kwa akili. Pamoja na mazoezi tosha na mapumziko, yatupasa kuchagua lishe yenye afya sana kadiri inavyowezekana na kuepuka vyakula visivyo najisi, vilivyotajwa katika maandiko matakatifu. Kwa vile vinywaji vya vileo, tumbaku na matumizi mabaya ya madawa hudhuru miili yetu, yatupasa kuepukana nayo pia. Badala yake yatupasa kujishughulisha na chochote kile kitakacholeta mawazo yetu na miili yetu yawe katika nidhamu ya kistro, ambaye hutamani uzima wetu, furaha, na wema. (Warumi 12:1-2, 1 Yoh 2:6, Waef 5:1;21, Wafil 4:8, 2 Wakor 10:5, 6:14, 7:1, 1 Pet3:1-4, Walawi 11:1-47, 3 Yoh. 2)

23. Ndoa na Familia

Ndoa ilianzishwa Edeni na Mungu na ikathibitishwa na Yesu kuwa muungano wa maisha yote kati ya mwanaume na mwanamke katika wenzi wenye upendo. Kwa mkristo kifungo cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na kishirikiwe tu na wenzi wenye imani moja. Upendo wa hiari, heshma, staha, na uwajibikaji ndizo fito za {kujenga}uhusiano huu, ambao utaakisi upendo, utakatifu, ukaribu, uthabiti wa uhusiano kati ya kristo na kanisa lake. Kuhusu talaka, Yesu alifundisha kwamba mtu anayemwacha mwenza, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, na akaoa {au kuolewa} na mwingine azini. Ingawa baadhi ya mahusiano ya kifamilia huenda yakashindwa kufikia lengo, wenzi katika ndoa ambazo wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa mwenzake katika kristo wanaweza kufaulu kufikilia katika umoja wenye upendo kupitia uongozi wa Roho na malezi ya kanisa. Mungu hubariki familia na anakusaidia kwamba washirika wake watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu kamili. Wazazi wawalee watoto wao katika kumpendeza na kumtii Bwana. Kwa kielelezo chao na maneno yao wawafundishe kwamba kristo ni mtiishaji mwenye upendo, daima mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe kiungo katika mwili wake, familia ya Mungu. Kukuza ukaribu wa mahusiano wa kifamilia ni moja wapo ya alama ya {kujulisha} ujumbe wa mwisho wa injili. (Mwa 2:18-25, Math 19:3-9, Yoh 2:1-11, 2 Wakor 6:14, Waef 5:21-33, Luka 16:18, 1 Wakor 7:10-11, Kut 20:12, Kumb 6:5-9, Mith 22:6, Mal 4:5-6)

24. Huduma Ya Kristo Katika Hekalu La Mbinguni

Kuna hekalu mbinguni, hema la kweli lililosimamishwa na Bwana na siyo mwanadamu. Ndani yake kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha kupatikana kwa ajili ya waumini fanaka za kafara yake ya upatanisho iliyotolewa mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa kuhani wetu mkuu na akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka 1884, mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku 2300, aliingia katika awamu ya pili nay a mwisho katika huduma yake ya upatanisho. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi ambaya ni sehemu ya mwisho ambayo hatimaye itakomesha dhambi yote, iliyokuwa mfano wa kutakaswa kwa hekalu la kale la waebrania katika siku ya upatanisho. Katika huduma hiyo kielelezo hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa kafara, likini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamilifu ya damu ya Yesu. Hukumu ya upelelezi kufunua kwa viumbe wa mbinguni ni nani miongoni mwa wafu wamelala katika kristo na hivyo, katika yeye wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika ufunuo wa kwanza. Pia inadhihirisha zazi ni nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani ya kristo, wakishika amri za Mungu na imani ya Yesu, na katika yeye, hivyo basi, wako tayari kwa ajili ya kuhamasishwa kuingia katika ufalme wa milele. Hukumu hii huthibitisha haki ya Mungu, katika kuwokoa wale wanaomwamini Yesu. Hutangaza kwamba wale waliohudumu kuwa watiifu kwa Mungu watapokea ufalme. Hitimisho ya huduma hii ya kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufunga mlango wa rehema ya mwanadamu kabla ya marejeo ya Yesu. (Waebr 8:1-5, 4:14-16, 9:11-28, 10:19-22, 1:3, 2:16-17. Dan 7:9-27, 8:13- 14, 9:24-27. Hes 14:34. Ezekl 4:6 Ufu 14:6-7, 20:12, 14:12, 22:12. )

25. Kuja Kwa Kristo Mara Ya Pili

Kuja kwa kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la kanisa, hitimisho kuu la injili. Kuja kwa mwokozi kutakuwa halisi, binafsi, kutaonekana kwa dunia mzima. Atakaporudi wenye haki waliokufa watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu na kuchukuliwa kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa sehemu nyingi za unabii, pamoja na hali ya sasa ya ulimwengu, huonyeshe kwamba kuja kwa kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote. .(Tito 2:13, Math 24, Mdo 1:9-11, Math 24:14, Ufu 1:7, 14:14-20, Math 24:43-43, Wakor 15:51-50, 1 Wathes 1:7, 4:13-18, 5:1-6, Marko 13, Luka 21:2, Tim 3:1-5).

26. Mauti NA Ufufuo

Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke yake hapatwi na mauti, atawapa uzima wa milele waliokombolewa wake. Mpaka siku hiyo mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kwa watu wote. Wakati kristo, aliye uzima wetu, atakapotokea, wenye haki waliofufuliwa na walio hai watafikwa utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki Bwana wao. Ufufuo wa pili ambao ni ufufuo wa waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye. (Warum 6:23, 1 Tim 6:15-16, Mhu 9:5-6, Zab 149:3-4, Yoh 11:11-14, 1 Wakor 15:51-54, 1 Wathes 4:13-17, Ufu 20:1-10)

27. Milenia {Miaka Elfu} na Mwisho wa Dhambi

Milenia ni miaka elfu moja ya utawala wa kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati ya ufufuo wa kwanza na pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa, dunia itakuwa ukiwa na utupu, bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na shetani na malaika zake. Mwishowe kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu watashuka kutoka Mbinguni. Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao pamoja na shetani na malika zake watauzingira mji, Lakini moto kutoka mbinguni utawateketeza ili kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu utakuwa huru bila dhambi na wenye dhambi milele. (Ufu 20, 1 Wakor 6:2-3, Yer 4:23-26, Ufu 21:1-5, Mal 4:1, Ezekieli 28:18-19)

28. Dunia Mpya

Katika dunia mpya, ambamo haki hukaa,Mungu ataweka tayari makao ya milele waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na kujifunza mbele zake. Kwa hapa Mungu mwenyewe atakaa pamoja na watu wake, na taabu na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na dhambi haitakuwepo tena. Vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai vitatangaza kwamba Mungu ni pendo, naye atatawala milele. Amina. (2 Pet 3:13, Isa 35, 65:17-25, Math 5:5, Ufu 21:1-7, 22:1-5, 11:5).